The House of Favourite Newspapers

Siku Moja Baada ya Kifo cha Binti Yake, Mama wa Carrie Fisher Naye Aaga Dunia

debbie-reynolds-photos-3IKIWA ni siku moja tu tangu mwanaye (Carrie Fisher) apatwe umauti kwa matatizo ya moyo wakati akiwa safarini kutoka London, Uingereza kwenda Los Angeles, Marekani, Msanii wa Hollywood Debbie Reynolds amefariki dunia jana Jumatano, Desemba 28, 2016 akiwa na umri wa miaka 84.

Debbie Reynolds ambaye ni mama mzazi wa marehemu Carrie Fisher, alikimbizwa hospital baada ya kushikwa na ugonjwa akiwa nyumbani kwa mtoto wake wa kiume Todd huko Beverly Hills.

carrie-fisher-mother-dead3Debbie Reynolds na mwanaye, Carrie Fisher ambao wote kwa sasa ni marehemu.

Debbie Reynolds ama Mary Frances, umaarufu wake ulikuwa mwaka 1952, wakati alipofanya tamasha sambamba na Gene Kelly katika wimbo uliojulikana kama ”..Singin’ in the Rain..”

Debbie aliachana na mumewe Eddie Fisher mwaka 1959 baada ya mume huyo kuingia kwenye mahusiano na mwanamke mwingine, Elizabeth Taylor. Debbie aliolewa mara mbili zaidi mwaka 1960 na 1984.

Alifanya vizuri kwenye tasnia ya uigizaji hasa wa vichekesho kwenye sinema ya “Tammy and the Bachelor” iliyokuza jina lake na “The Unsinkable Molly Brown” ambayo alishinda Tuzo ya Oscar.

Ilikupita hii?==>Aliyecheza Filamu ya Kivita ya Star Wars, Carrie Fisher Aaga Dunia

Would You? – Singin’ in the Rain – Debbie Reynolds own voice

Darasa Asepa na Kijiji Ilala, Aonjesha Mashabiki Shoo Kali ya Bure!

Comments are closed.