Ofisa Masoko wa Global, Songolo Bilal (katikati) akiwaelekeza namna ya kujaza kuponi za kushiriki bahati nasibu ya shinda gari.
Zikiwa zimesalia dakika za lala salama kwa msomaji wa magazeti ya bora ya michezo yanayoongoza kwa habari za uhakika zilizofanyiwa uchunguzi wa kina ,Championi na Spoti Xtra, kujinyakulia gari aina ya Toyota Fun Cargo jana Alhamisi maofisa wa idara ya Masoko na Usambazaji waliendelea kuwasisitiza wasomaji hao kushiriki bahati nasibu hiyo.
Kitengo cha Masoko na Usambazaji cha magazeti hayo, jana kiliingia mitaani maeneo mbalimbali ya jiji la Dar ikiwemo Manzese, Magomeni na Mwananyamala na kuzidi kuwahamasisha wasomaji hao kuendelea kushiriki Bahati Nasibu hiyo na kuweza kunyakua gari hilo.
Wasomaji hao walionekana kuhamasika na kuonekana kuyachangamkia magazeti hayo na kujaza kuponi inayoelekeza jinsi ya kushiriki shindano hilo.
Akizungumza na wasomaji hao, Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji, Anthony Adam aliwaambia wasomaji hao kuwa mshindi huyo anatarajiwa kupatikana mapema wiki ijayo.
Anthony amesema katika kumsindikiza mshindi wa gari hilo zitachezeshwa droo nyingine ambapo washindi wa zawadi mbalimbali kama vile simu za kisasa za mkononi (smart phone) pesa taslimu na nyinginezo nao watapatikana.
Anthony aliwasisitiza wasomaji hao kuchana kuponi iliyopo ukurasa wa pili kwenye magazeti hayo na kumkabidhi muuza magazeti yeyote aliye karibu nao kwa ajili ya kuweza kujishindia gari na zawadi hizo.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL