The House of Favourite Newspapers

Sikukuu ya Idd 2017

0

SIKUKUU ya Iddi el Fitri nchini, kama ambavyo imekuwa ikitokea kila mara,  kwa waumini wa Kiislam,  baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan,  leo imeadhimishwa na wafuasi wa Answar Sunna .

Kwa upande mwingine sikukuu hiyohiyo kiserikali,  kupitia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), itaadhimishwa kesho Jumatatu na keshokutwa Jumanne.  Hivyo kitaifa kesho na keshokutwa ni siku za mapumziko kwa Watanzania wote, ikiwa Idd Mosi na Idd Pili.

Ni siku ambayo Watanzania wataungana na ndugu zao wa madhehebu ya Kiislam kuadhimisha kumalizika kwa moja ya nguzo muhimu za imani yao.  Sikukuu hiyo kitaifa itaadhimishwa  Mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, menejimenti na wafanyakazi wote wa kampuni hiyo, wanawatakia Watanzania wote sikukuu njema na mapumziko ya amani katika kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kiroho.

 

Leave A Reply