The House of Favourite Newspapers

Silinde Amvua Madaraka Mwalimu Mkuu Ikhanoda – Video

0

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala wa Mikoa na  Serikali za Mitaa (Tamisemi), David Silinde, amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ikhanoda Kata ya Ikhanoda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Omary Selestine, baada ya kugundua kuwa amefanya matumizi mabaya ya fedha za umma katika ujenzi wa bwalo la chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.

 

Amefanya maamuzi hayo alipotembelea shule hiyo kukagua mradi wa ‘lipa kutokana matokeo’ (EP4R) ambao shule hiyo walipewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo lakini mpaka sasa fedha zaidi ya sh. milioni 50 zimetumika huku ujenzi ukiwa bado upo katika hatua ya msingi.

 

Silinde amebaini ubadhirifu mkubwa wa fedha huku baadhi ya vifaa vya ujenzi wa mradi huo vikinunuliwa kwa bei ya kubw kuliko uhalisia wa bei ya kawaida, hivyo kumkabidhi mwalimu huyo polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili wamhoji huku pia akivunja bodi ya shule na kumvua madaraka mtendaji aliyekuwa akisimamia ujenzi huo.

“HUYU NI MWIZI KAMA WEZI WENGINE, POLISI ONDOKENI NAE” – NAIBU WAZIRI SILINDE

 

Leave A Reply