visa

Silvia Alivyotwaa Taji la Miss Tanzania 2019

Mrembo Silvia Sebastian mkazi wa Buhongwa  jijini Mwanza (katikati) akiwapa ‘hi’ wageni waalikwa baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Mrembo Silvia Sebastian mkazi wa Buhongwa Mwanza ambaye pia alitwaa taji la Miss Mwanza na Miss Lake Zone mwaka huu usiku wa kuamkia leo ametwaa taji la Miss Tanzania katika kinyang’anyiro kilichowashirikisha warembo ishirini kutoka mikoa na kanda mbalimbali hapa nchini.

Warembo wakitoa shoo.

Kinyanganyiro hicho kilifanyika Jengo la LAPF Tower Kijitonyama Dar na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mashindano akiwemo waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

 

Sambamba na Mwakyembe ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi pia alikuwepo Waziri wa Utalii mstaafu, Waziri Lazaro Nyarandu.

Silvia katika vazi la jioni kabla ya kutangazwa mshindi. 

Waziri Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Lazaro Nyarandu.

Mmoja kati ya majaji, Angela Damas akieleza sifa za mshindi anayetakiwa kabla ya kupatikana.

Akili The Brain (kulia) na kundi lake wakitoa burudani.

Hawa ndiyo walioingia kumi bora.

Hii ndiyo tano bora.

Silivia na Queen Mungesi ambaye aliishia mshindi wa pili wakiwa wameshikana mikono wakati akisubiliwa mshindi kati yao.

Waziri Mwakyembe akimkabidhi, Silivia hundi ya milioni kumi baada ya kutwaa taji.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Toa comment