The House of Favourite Newspapers

SIMANZI! Mwili wa Isaac Gamba Waagwa Mwanza, Wasafirishwa Bunda

SIMANZI NA MAJONZI! MWILI wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba umeagwa katika Viwanja vya Ofisi za Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari (UTPC) jijini Mwanza leo Jumanne, Oktoba 30, 2018.

Mwili wa Gamba ambao uliwasili jana nchini na kuagwa katika Hospitali ya Lugalo jijini Dae re Salaam kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Mwanza, umewasili jijini humo leo Jumanne, Oktoba 30, 2018 asubuhi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa Gamba ambapo baada ya kuagwa jijini Mwanza, mwili huo tayari umesafirishwa kwenda nyumbani kwao wilayani Bunda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Marehemu  hakuwahi kuugua ugonjwa wowote wa kuaminika zaidi ya kukutwa akiwa amefariki chumbani kwake Alhamisi, Oktoba 18, mwaka huu, jijini Bonn nchini Ujerumani alikokuwa akifanya kazi zake.

Baada ya uchunguzi wa hospitali nchini Ujerumani, imegundulika kuwa kilichosababisha kifo chake ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo (Brain Hemorrhage) yaani presha ya damu.

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

MWILI WA ISAAC GAMBA UKIAGWA MWANZA LEO

Comments are closed.