The House of Favourite Newspapers

ads

Simba 1-3 Jwaneng (Agg: 3-3) SIMBA OUT Ligi ya Mabingwa

0


Baada ya ushindi wa 0-2 ugenini, Simba wapo dimbani kuumana na Jwaneng Galaxy katika mchezo wa pili wa hatua ya pili ya ligi ya mabingwa wa Afrika.

Jwaneng Galaxy hawana masihara, wanafunga goli la pili dhidi ya Simba. Wanahitaji goli moja kuwa sawa. Simba SC 1-2 Jwaneng Galaxy Agg: ( 3-2 )

60’: Simba 1-2 Jwaneng (Agg: 3-2).

55’: Simba 1-1 Jwaneng (Agg: 3-1).

47′: Simba 1-1 Jwaneng (Agg: 3-1).

Rally Bwalya anaitanguliza Simba dakika ya 41. Simba 1-0 Jwaneng (Agg: 3-0).

 

Kwa Mashine hizi… Waswana Wanatokea wapi?

KOCHA Msaidizi wa Simba, Hitimana Thierry, amefunguka kuwa kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa kwenye Dimba la Mkapa, Dar, wataingia na mbinu ya kucheza soka la kushambulia na pasi nyingi ili kujihakikishia kutinga hatua ya makundi.

 

Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Oktoba 17, mwaka huu nchini Botswana ambapo katika mchezo huo Simba walionekana zaidi kucheza soka la kujilinda tofauti na ilivyozoeleka wakicheza soka la kuvutia maarufu pira biriani.


Ukiangalia mashine za
Simba zilivyokamilika, ni wazi Waswana hao hawana pa kutokea leo.Mashine za Simba ambazo zinatarajiwa kuanza katika mchezo wa leo ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Henock Inonga,Pascal Wawa, Taddeo Lwanga, Hassan Dilunga, Sadio Kanoute, John Bocco, Rally Bwalya na Bernard Morrison.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Hitimana alisema malengo yao kwenye mchezo wa kwanza ilikuwa ni kupata ushindi kwanza na si kucheza soka la kuvutia jambo ambalo walifanikiwa, huku akitamba kuwa kwenye mchezo wa leo mashabiki wa timu hiyo watarajie kuona pira biriani kama walivyoizoea timu yao ikicheza.


“Malengo yetu kwenye
mchezo wa kwanza ilikuwa ni kupata ushindi jambo ambalo tulifanikiwa tukapata mabao ya haraka, hatukuwa na mpango wa kucheza soka la kufurahisha watu bali tulizingatia zaidi matokeo kwani mechi za hatua ya mtoano matokeo ndiyo kitu cha kwanza.

 


“Kwenye mchezo wetu
wa kesho (leo) tutaingia na mbinu tofauti, kwanza kabisa ni kutafuta matokeo, pili
ni kucheza soka la kuvutia
ambalo limezoeleka kwa mashabiki wetu, wachezaji wako tayari, hivyo mashabiki wetu watarajie ushindi.”

NA LUNYAMADZO MLYUKA NA HUSSEIN MSOLEKA, DAR

Leave A Reply