The House of Favourite Newspapers

Simba, Azam Watoshana Nguvu

0

Azam FC na Simba SC wamegawana point moja kila mmpja katika Dimba la Chamazi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jioni hii.

Azam ndiye alikuwa wa kwanza kupata bao dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia kwa Idd Nado dakika ya 43.

Simba walisawadhisha dakika za lala salama kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa Rwanda, Meddie Kagere dakika ya 84.

Simba tayari wameshatangazwa kuwa mabingwa kwaara ya nne mfurulizo huku wakofuatiwa na Yanga ambaye naye leo ameshinda mbele ya Ihefu kwa bao 2-0, mabao yaliyofungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Nafasi ya tatu inashikwa na waoka mikate, Azam FC na imebaki mechi moja kwa kila timu kukamilisha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Leave A Reply