The House of Favourite Newspapers

Simba Kuchagua Mwenyekiti Kesho

0

KLABU ya soka ya Simba leo Februari 06, wameitisha mkutano na wanahabari kuzungumzia mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo utakaofanyika kesho Februari 7 2021.

 

Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba, Boniface Lihamwike amesema wanachama wawili ndio watakaopigiwa kura ili kumpata mwenyekiti mpya wa klabu hiyo.

“Kesho utafanyika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Simba wa wanachama, wagombea wawili ndio watachuana kesho Murtaza Mangungu na Juma Nkamia. wanachama wanatakiwa kujua hao ndio watawapigia kura”

 

Aidha amesema moja ya kigezo cha kupiga kura ni mwanachama kulipia ada ya uanachama hivyo kesho nje ya ukumbi wa mkutano kutakuwa na eneo maalumu ambalo watatumia wanachama ambao hawajalipa kufanya malipo.ameongoza  Lihamwike.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply