The House of Favourite Newspapers

Serikali: Hakuna Mgonjwa wa Corona Bugando, Sekou-Toure

0

SERIKALI imesema hakuna wagonjwa wa corona katika hospitali ya Kanda ya Bugando na ile ya rufaa ya Sekou-Toure za jijini Mwanza.

 

Hayo yalisemwa jana Ijumaa Februari 5, 2021 katika mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Mabula Mchembe, na waandishi wa habari huku akiwataka wananchi kutokuwa na hofu.

 

Mchembe alitembelea hospitali hizo ili kupata ukweli kama zina wagonjwa hao ama la baada ya madai hayo kusambaa mitandaoni. Awali akitoa taarifa kwa katibu mkuu huyo, kaimu mkurugenzi wa Bugando, Dk Fabian Massaga, amesema hospitali hiyo haina mgonjwa yeyote wa Covid-19 kama inavyodaiwa.

 

Amesema wagonjwa wanaopokelewa ni wale wenye changamoto ya kupumua inayotokana na maradhi mengine ikiwemo shinikizo la damu, uzito uliopitiliza na kifua kikuu. Maelezo kama hayo pia yalitolewa na mganga mfawidhi wa Sekou-Toure, Dk Bahati Msaki, aliyesema “tunao wagonjwa watano wenye changamoto ya kupumua inayotokana na maradhi mengine.”

 

Naye,  Massaga amesema kuwa, Hospitali ya Bugando inapokea wagonjwa wa aina mbalimbali wakiwemo wagonjwa wenye matatizo ya kupumua kama vile magonjwa ya pumu, magonjwa ya kisukari, magonjwa ya presha na mshtuko.

 

 

“Sio kweli kuwa, Hospitali ya Bugando imejaa wagonjwa wa matatizo ya kupumua, na siyo kweli wodi zimejaa wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, ukweli ni kwamba tunawapokea wagonjwa wa aina mbalimbali ambayo yanapelekea kuwa na matatizo katika mfumo wa hewa, mfano wenye magonjwa ya pumu na kisukari, alisisitiza hilo,” alisema  Massaga.

 

 

Leave A Reply