The House of Favourite Newspapers

Simba kuwaweka kikao Bwalya, Chama

0

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba, amesema kuwa watafanya kazi kubwa kwa wapigaji mipira iliyokufa ambayo wanaipata katika mechi ambazo wanacheza.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Matola alisema kuwa tatizo la kushindwa kupata matokeo mazuri lina maumivu makubwa na wamegundua tatizo lilipo ikiwa ni pamoja na kushindwa kutumia mipira ya kona na faulo.

“Kushindwa kupata matokeo mazuri kwa Simba ni maumivu lakini tumegundua kwamba suala la kukosa kutumia mapigo huru, hilo nalo ni kosa, hivyo kwa wapigaji wa kona na faulo wote tutazungumza nao ili kuboresha makosa yetu.

“Ikiwa kwenye mechi tunapata kona zaidi ya 9 na hazileti mabao, hilo ni jambo la kufanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi, bado tupo imara na makosa kila siku tunayafanyia kazi na tutazungumza na wachezaji wetu ili tuweze kupata ushindi pia kupitia mapigo hayo.

“Mfano kwenye mchezo dhidi ya Prisons tulipata kona tatu ziliweza kuwa na hatari kwenye lango la mpinzani lakini hatukufunga, bado kuna mechi zinakuja tunaamini tutafanya vizuri,” alisema Matola.

Wapigaji kona wa Simba ni Rally Bwalya, Clatous Chama, Sadio Kanoute na Bernard Morrison ambaye amesimamishwa kwa muda kutokana na masula ya nidhamu.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Leave A Reply