The House of Favourite Newspapers

Muu Flow Awatisha Mastaa

0

KINDA anayekuja kwa kasi kunako anga la muziki wa kufokafoka (Hip Hop), Muu Flow ni mdogo wa umri, lakini mkubwa wa maarifa kwani amewatisha baadhi ya wasanii kutokana na mambo anayoyafanya kwenye muziki wake.

 

Akizungumza na IJUMAA SHOWBIZ, Muu Flow ambaye kwa sasa anatamba na kichupa chake cha Swing Swing anasema kuwa, anataka kufanya mapinduzi wa muziki wa Hip Hop maana anaona kama wamepona.

 

“Najua wengi wanajiuliza mtoto mdogo hivi anawezaje kuwakalisha watu wazima, ila nataka kuwaambia mimi ni mdogo wa umri tu, lakini mkubwa wa maarifa.

 

“Kingine nataka kufanya mapinduzi kwenye muziki wa Hip Hop Bongo maana naona kama kumepoa f’lani hivi wasanii wakubwa wanashindwa kuutendea haki muziki huu na kwa sasa nipo njiani kuachia project, mimi ni kazi juu ya kazi watajua hawajui,” anasema Muu Flow.

STORI: KHADIJA BAKARI

Leave A Reply