The House of Favourite Newspapers

Simba Mabingwa Wa Ngao Ya Jamii, Yaipiga Mtibwa Bao 2-1

TIMU ya Simba leo imefanikiwa kutetea taji lake la mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu, Ngao ya Jamii kwa kuifunga Mtibwa Sugara ya Morogoro mabao 2-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

Simba waliweza kujipatia mabao yake kupitia kwa wachezaji wake waliowasajili katika dirisha kubwa la usajili, Meddie Kagere na Hassan Dilunga, kwa sasa Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne huku wapinzani wao Yanga wakishika nafasi ya kwanza kwa kuchukua mara tano.

Comments are closed.