The House of Favourite Newspapers

Simba Wakutana Fasta Kujadili Bil 2 za Mo

0

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’

UONGOZI wa juu wa Klabu ya Simba umepanga kukutana ndani ya siku mbili hizi ili kujadili na kupanga wapi wataanzia mpango wa kujenga uwanja wao wa nyumbani kama alivyoshauri mwekezaji,Mohamed Dewji (Mo Dewji).


Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’
akieleza kuwa
kitendo cha Mo kusema atatoa Bil 2 kwa ajili ya kujenga uwanja siyo cha
kulazia damu na wanatakiwa
kukutana haraka kuanza kutekeleza.


Mo, kupitia ukurasa
wake wa Instagram juzi aliandika kuwa: “Nimepokea maoni mengi ya Wanasimba
wenzangu wakishauri tujenge
uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo.

“Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili. Naomba Bodi ya Simba kukaa
na kuja na utaratibu wa haraka
ili jambo hili lianze utekelezaji.


“Kwa kuanza naahidi
kuchangia Tsh. 2 bilioni. Nawaomba Wanasimba tuchangie sote.” Akizungumzia ombi la Mo la kuitaka Bodi ya Simba ikutane na kuja na utaratibu wa kuanza zoezi hilo, Try Again alisema: “Kimsingi neno lake limekuwa kubwa kwa Wanasimba wote na sisi kama bodi tutakutana haraka ili
kuweza kujadili suala
hilo.


“Binafsi nilikuwa
natamani sana kuona siku nikiwa naondoka Simba niwe nimeacha alama ambayo itafanya nikumbukwe na Wanasimba wote, hivyo kwa haraka sana tutaanza mchakato baada ya viongozi kukubaliana.”
Kauli ya Mo ilikuja baada
ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kudai kuwa amezuiwa kuingia Uwanja wa Mkapa kushuhudia mechi ya Simba dhidi ya Yanga

STORI: Issa Liponda, Chapioni Jumatano

Leave A Reply