The House of Favourite Newspapers

Simba walia Yanga SC kuondolewa na Zanaco

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kitendo cha Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kimewaumiza sana.

Yanga ilitupwa nje katika michuano hiyo na Zanaco ya Zambia baada ya kutoka sare ya bao 1-1 hapa nyumbani na kwenda Zambia ambako wikiendi iliyopita walitoka suluhu na hivyo kuondolewa kwa bao la ugenini.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Simba ambao ni mahasimu wakubwa wa Yanga, umedai kuwa umesikitishwa vilivyo na hali hiyo kwani ni pigo kubwa kwa soka la Tanzania.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, ameliambia Championi Jumatano kuwa, uongozi wa timu hiyo haukupenda Yanga itolewe katika michuano hiyo, kwa sababu ilikuwa ikiwakilisha nchi, hivyo kutolewa kwao ni pigo kubwa kwa taifa.

“Sisi kama Simba hatukufurahishwa kabisa na hali hiyo iliyowatokea Yanga, kwani tumeumia tukiwa kama Watanzania ambao tulikuwa tukiiombea ifike mbali katika michuano hiyo hata hivyo wamepata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, wajipange vilivyo na kuufanyia kazi upungufu wote uliojitokeza kwenye mechi dhidi ya Zanaco,” alisema Kaburu.

Na Sweetbert Lukonge/CHAMPIONI/GPL

Comments are closed.