The House of Favourite Newspapers

Kamanda Sirro: Tukio la RC Makonda Kuvamia Clouds Media Sijalipata Bado (VIDEO)

DAR ES SALAAM: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema hajapata taarifa rasmi kuhusu kuvamiwa kwa wafanyakazi wa Clouds Media Group na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda usiku huku akiwa na askari.

“Swala hilo hata mimi nalisikia tu kwenye mitandao ya kijamii lakini halijafika kwangu rasmi, nadhani ni jambo kubwa hivyo niwasihi watendewa ambao ni Clouds Media wafike kwenye kituo cha polisi na kuripoti uvamizi huo haraka.”

“Kama wameripoti Kituo cha Osterbay mimi sijapata maandishi kutoka kwa RPC wa Kinondoni kuhusu tukio hilo, hivyo naweza kusema bado halijafika ofisini kwangu.” Alisema Sirro.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anadaiwa kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds TV na kudaiwa kushinikiza kurushwa hewani kwa kipindi chake jambo lililoleta mtafaruku na taharuki miongoni mwa wafanyakazi wa Clouds na Wananchi kwa ujumla.

Aidha leo Machi 22, kamati iliyoundwa na Waziri Nape Nnauye umebaini kuwa sababu ya uvamizi huo ni habari iliyodaiwa kumuhusu mwanamke aliyedai kuzaa na Mchungaji Josephati Gwajima ambapo alitaka habari hiyo iruke kwenye kipindi..

Comments are closed.