The House of Favourite Newspapers

Simba Wamtunuku Mo Dewji Tuzo Ya Heshima, Zimbwe Naye Apewa Tuzo Yake

0
Tuzo maalum ya heshima kwa mwanachama wa muda mrefu wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ .

Kundi la mtandaoni la WhatsApp la Simba HQ,  limetoa  tuzo maalum ya heshima kwa mwanachama wa muda mrefu wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutokana na mchango wake katika klabu hiyo kwa jumla.

Tuzo hiyo ilitolewa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Simba HQ iliandaa futari kwa wadau wao ikiwa ni pamoja na kuzungumza jinsi msimu wa 206/17 ulivyokuwa ambapo Simba ilimaliza kwa kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Vocacom pamoja na kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.

Mohammed Dewji ‘Mo’.

Mo alipewa tuzo hiyo lakini hakuwepo ukumbini hapo, ambapo alitumia ukurasa wake wa Instagram kushukuru kwa tuzo hiyo.

Awali alianza kwa kuonyesha picha ya tuzo na kuandika: “‪Ninashukuru na ni heshima kubwa kwangu kupokea hii tuzo kutoka kwa wapendwa wangu Klabu ya Simba.”

Baada ya muda akaweka picha akiwa ameshika tuzo hiyo, na kuandika “I am deeply honored and humbled to have been presented this our by my beloved club Simba S.C #SimbaNguvuMoja #NguvuMoja”

Aidha, mkusanyiko huo ulitumika kumpatia tuzo Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ au Zimbwe Jr ya Mchezaji Bora wa Msimu wa 2016/17 klabuni hapo, pia Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Simba ilienda kwa Dennis Kitandu.

Leave A Reply