The House of Favourite Newspapers

Simba Wapewa Siri za Wabotswana

0

SIMBA huenda wasipate ushindani mkubwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na wapinzani wao Jwaneng Galaxy kukosa mechi nyingi za ushindani.

 

Jwaneng Galaxy ya Botswana ni timu ambayo imekosa mechi nyingi za ushindani kutokana na Ligi Kuu ya Botswana kusimama kwa muda mrefu kutokana na athari za corona.

 

Kiungo Mtanzania Abdallah Hamis ambaye anakipiga Orapa United ya Botswana alisema moja ya sababu ambazo huenda zikawasaidia Simba kupenya kirahisi ni kwa sababu wapinzani wao hawachezi ligi na wanafanya zaidi mazoezi.

 

Kocha Mkuu wa Jwaneng Galaxy, Morena Ramoreboli, alikiri kuwa kuna ugumu wa kupenya mbele ya Simba kwa kuwa wana kikosi bora na wamepata mechi nyingi za kucheza tofauti na wao.

 

Wakati kocha huyo akisema hivyo, kiungo wa timu hiyo, Ricardo Lourenco amesema: “Simba tumewafuatilia baada ya kujua tutacheza nao, hivyo kiasi chake tunajua wanapenda kucheza soka la pasi nyingi za chini kitu ambacho kitasaidia katika mechi yetu dhidi yao. “Tunawaheshimu lakini tunachokiangalia ni kupata matokeo mazuri dhidi yao.”

ISSA LIPONDA NA IBRAHIM MUSSA

Leave A Reply