The House of Favourite Newspapers

Simba Yaendeleza Dozi, Yainyuka Ruvu Shooting Kirumba

0

MABINGWA Watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba, imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting, katika mchezo uliochezwa leo Juni 3, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

 

Simba  iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa goli 1-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza kwenye uwanja wa Mkapa Dar.

 

Nahodha John Bocco, alikuwa wa kwanza kuanza kucheka na nyavu baada ya kupachika bao dakika ya 17 ambalo lilidumu mpaka mapumnziko.

 

Kipindi cha pili licha Ruvu Shooting kusaka bao la kusawazisha ni Simba waliowainua maelfu ya mashabiki baada ya Chris Mugalu kuweka kambani bao la pili dakika ya 61.

Bocco kwa mara nyingine akapachika goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

 

Wachezaji wa Ruvu Shooting  wawili walitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu katika nyakati tofauti, beki Juma Nyoso na Mlinda mlango Abdalah Rashidi.

 

Simba imefikisha alama 67 ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza michezo 27, Yanga nafasi ya pili na alama 61 baada ya michezo 29.

Leave A Reply