The House of Favourite Newspapers

Simba Yaifanyia Umafia Yanga, Yaondoka na Nyota Wawili

0

KLABU ya Simba inasemekana baada ya kufungwa na Yanga, Julai 3, 2021 imeanza kuifanyia umafia timu ya Yanga, kwa kuwasainisha nyota wawili ambao walihitajika na Yanga kwa ajili ya msimu Ujao wa Ligi pamoja na michuano ya Kimataifa.

 

Simba inasemekana kwamba imeifanyia umafia kwa kuwasainisha nyota wawili akiwemo Jeremiah Kisumbi kutokea Tanzania Prisons na Kimbu Denis kutokea Mbeya City zote kutokea Jijini Mbeya. Inasemekana kwamba Simba hasira zote kwa sasa zimehamia katika usajili kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi Chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi yaani 2021/2022.

 

Hapo awali taarifa zilitoka kwamba Jerimiah Kisubi alikuwa katika hatua za mwisho kumalizana na Yanga. Lakini pia Kimbu Denis nae alisemekana kwamba alikuwa na mazungumzo na Yanga. Lakini karata imegeuka na sasa hivi taarifa zinaitaja Simba imeanza mazungumzo na nyota hao na huenda wakati wowote wakatangazwa kutua ndani ya Simba.

 

Kwa Sasa Simba pia inatajwa katika nyota kadhaa wa kimataifa kutokea katika nchi mbalimbali akiwemo Khalid Aucho, Mosesi Phiri, Walter Bwalya pamoja na nyota wengine kadhaa wa kadha ambao wanatakiwa kuja kuimalisha kikosi cha wekundu wa Msimbazi yaani Simba.

 

Simba kupitia kwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji aliwahi kunukuliwa akisema kwamba. Simba inahitaji kufanya usajili wenye tija kubwa kwa ajili ya kukifanya kikosi cha Simba kiwe Imara zaidi kwa ajili ya michuano ya ndani na hata nje ya nchi ya Tanzania.

 

Unatoa maoni gani kwa taarifa hizo ambazo zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya tetesi hizo juu ya nyota hao ambao wanatajwa kusajiliwa na Simba. Weka maoni yako hapo chini bila kusahau Kufollow ili uendelee kupata habari kila siku kupitia channel hii.

 

Leave A Reply