The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Tumedhamiria Kuendeleza Zao La Zabibu

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Julai 5, 2021 ametembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) katika eneo la uzalishaji miche ya zabibu, mashamba na viwanda vya kuchakata zabibu, Dodoma.

 

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendeleza zao la zabibu na kuhakikisha linaleta tija kwa wakulima.

“Serikali imeanzisha kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la zabibu, tunataka kumsaidia mkulima kuanzia maandalizi ya shamba, upatikanaji wa pembejeo hadi hatua ya mauzo.”

 

Katika kuhakikisha kilimo hicho kinapata mafanikio, Waziri Mkuu amezitaka taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) zibadilike na kutoa mikopo kwa wakati.

 

Kadhalika, Waziri Mkuu ametembelea skimu ya umwagiliaji ya mashamba ya wakulima wa zabibu iliyopo Hombolo na amewasisitiza wakulima walinde miundombinu hiyo.

Leave A Reply