The House of Favourite Newspapers

Simba Yaifunika Yanga Kwenye Idadi ya Hat trick Ligi Kuu Bara 2022/23

0

MASTAA wa Simba wamewafunika watani zao wa jadi Yanga kwenye idadi ya hat trick ambazo wamefunga ndani ya za Ligi Kuu Bara 2022/23.

Ni mastaa saba walifunga hat trick katika Ligi Kuu Bara, huku ikiwa ni watatu kutoka Simba, wawili kutoka Yanga, mmoja ni mali ya Namungo, aliyefunga kazi ni Prince Dube wa Azam FC.

Nyota wa kwanza kufunga hat trick msimu wa 2022/23 ni Fiston Mayele wa Yanga aliyefunga kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mwingine kufunga kutoka Yanga ni Stephane Aziz KI katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar, huku akifunga mabao mawili kwa mapigo ya penalti.

Kutoka Simba ni John Bocco mwenye hat tick mbili, aliwatungua Ruvu Shooting na Tanzania  Prisons, mechi zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

Jean Baleke wa Simba aliwatungua Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro. Mwingine ni Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ yeye anazo mbili, aliwatungua Tanzania Prisons ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya Simba akitokea Geita Gold, ile ya pili aliwatungua Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex.

Ibrahim Mkoko nyota wa Namungo aliwatungua KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru waliposepa na pointi zote tatu mazima.

Prince Dube alifunga kazi kwa kufunga hat trick kwenye mchezo wa mwisho Juni 9, Uwanja wa Azam Complex alipowatungua Polisi Tanzania mabao manne na kufikisha mabao 12.

Jumla ndani ya Simba hat trick zimefungwa tano, huku Yanga ikiwa imefunga mbili na Namungo wanayo moja kama ilivyo Azam FC.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA, CHAMPIONI

TUZO ya GOLI BORA na BEKI BORA ZAENDA YANGA, FISTON MAYELE na DICKSON JOB..

Leave A Reply