The House of Favourite Newspapers

Simba Yaipangia Azam Kikosi Kazi Asubuhi

0

KAMA ulikuwa hujui basi tambua kwamba kikosi cha Simba ambacho utakiona leo Jumatano kikipambana na Azam FC kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kilipangwa jana Jumanne asubuhi baada ya kocha wao Sven Vandenbroeck kupanga iwe hivyo.

 

Kocha huyo amesema kwamba kwa siku nzima ya Jumatatu hakuwa na mawazo na mechi hiyo kwa sababu ya kujipa muda wa kupumzika baada ya kurudi Dar wakitokea Mbeya ambapo walipambana kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara.

Sven ameliambia Championi Jumatano, kuwa:“Kitu cha kwanza tulipumzika ikiwa ni baada ya kuchukua ubingwa. Hatukuwa na ratiba yoyote ile zaidi ya kupumzika tu.

 

Uzuri ni kwamba kila mmoja yuko vizuri.“Asubuhi ya siku itakayofuata (jana Jumanne), ndiyo nitajua kikosi gani kitacheza dhidi ya Azam FC lakini pia kwa namna gani mbinu zangu ziwe na nitumie mbinu ipi kwenye mechi hiyo.“Lakini kitu kikubwa ni kuwa nataka ubingwa mwingine baada ya kutwaa ule wa Ligi Kuu Bara.

 

Hilo ndilo lengo letu kwa mwaka huu wa 2020, nataka kulitimiza na kuona tunatwaa makombe mawili,” alimaliza Sven.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

VITUKO! MORRISON AWAKIMBIZA MAKOMANDOO YANGA USIKU MNENE…

Leave A Reply