The House of Favourite Newspapers

ads

Simba Yamtangaza Imani Kajula Kuwa Afisa Mtendaji Mkuu Mpya (CEO)

0

KLABU ya Simba leo Januari 26, 2023 imemtangaza Imani Kajula kuwa Mtendaji Mkuu (C.E.O), ambaye anachukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyemaliza muda wake.

Imani Kajula ambaye alikuwa CEO wa EAG Group ambayo ni Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ana uzoefu wa kufanya kazi katika masuala ya masoko na biashara kwa zaidi ya miaka 20.

Imani hadi anatangazwa kujiunga na Simba alikuwa CEO wa EAG Group kuanzia 2013, kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano NMB (2006-2013), Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Tanzania Postal Bank (2003-2006) na alikuwa Meneja Masoko CRDB Bank (1999-2003).

NANI ni NANI MKEKA MPYA wa MA-DC wa RAIS SAMIA, WENGINE WAHAMISHWA WILAYA…

Leave A Reply