The House of Favourite Newspapers

ads

Alichokifanya mbele ya Nabi… Mamadou Doumbia Gumzo Yanga

0
Mamadou Doumbia

KAZI aliyopiga kwa siku chache alizofanya mazoezi na Yanga, kumemfanya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe afungue mdomo na kusema beki wao mpya, Mamadou Doumbia siyo mtu wa mchezo.

Doumbia alitua nchini Jumamosi iliyopita na kufanya mazoezi na timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, lakini bado hajaanza kucheza mechi, anatarajiwa kuonekana wikiendi hii wakati Yanga ikicheza mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Rhino Rangers.

Kamwe ambaye anamuita Doumbia kama beki la CHAN, alisema beki huyo hapendi kucheka akiwa anafanya kazi yake uwanjani na hiyo inawapa amani ya kuona wanakwenda kuzima vurugu zote kwenye eneo lao la ulinzi.

“Yule beki wa CHAN (Doumbia) ni hatari sana, hacheki na mtu kabisa, yeye anapiga kazi tu, yaani anakwenda kuwaonesha balaa uwanjani, yule ni beki aliyekamilika, huku mazoezini anazima kila aina ya shambulizi, hivyo msubirieni uwanjani,” alisema.

Doumbia alitambulishwa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu kati ya wachezaji wanne waliosajiliwa na timu hiyo kipindi hicho. Wengine ni Mudathir Yahya, Kennedy Musonda na Metacha Mnata.

Beki hiyo ni raia wa Mali na anacheza kwenye Timu ya Taifa ya Mali ambayo ilikuwa Algeria kwenye mashindano ya CHAN.

NANI ni NANI MKEKA MPYA wa MA-DC wa RAIS SAMIA, WENGINE WAHAMISHWA WILAYA…

Leave A Reply