The House of Favourite Newspapers

Simba: Yanga Tambeni, Msimu Ujao Mtatutambua

0
Kikosi cha timu ya Simba.

Na Omary Mdose | CHAMPIONI |GPL

SIMBA wamesikia tambo za Yanga baada ya kuwa na uhakika wa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kisha wakasema, tambo zao hizo mwisho msimu huu kwani msimu ujao itakuwa ni zamu yao.

Simba kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 65, huku Yanga ikiwa kileleni na pointi 68 ambapo leo kwenye mechi za kumaliza msimu, Yanga inaweza kupewa kombe lake.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wamekubali yote yaliyotokea katika ligi msimu huu, hivyo wanaandaa majeshi yao kwa ajili ya kutesa msimu ujao.

Wachezaji wa timu ya Yanga.

“Ukiangalia msimu huu tulianza vizuri lakini mwishoni tukapoteza mwelekeo kidogo, Yanga wakatupita na sasa wanaenda kukabidhiwa ubingwa ambao awali ilionekana sisi ndiyo tunaweza kuutwaa.

“Kama msimu uliopita tulimaliza nafasi ya tatu, msimu huu tunamaliza wa pili, basi tunaamini msimu ujao tutakuwa sisi wa kwanza na kuwa mabingwa, hilo linawezekana kabisa kama tukiongeza juhudi tulizozionyesha msimu huu.

“Yanga tambo zao zinaisha msimu huu, msimu ujao wasahau ishu ya ubingwa, tunaanza na Kombe la FA msimu huu, kisha msimu ujao tunachukua yote,” alisema Mayanja.

Leave A Reply