The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Wanapambana Na Hali Zao Kimataifa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho

0

MGAAGAA na upwa hali wali mkavu. Ipo hivyo, lakini kwenye anga za kimataifa, wali mkavu unaliwa kutokana na ugumu uliopo.

Simba rekodi yao ya kadi nne za njano kwenye mchezo mmoja dhidi ya Horoya, bado hawajaivunja, lakini Yanga wao nao wanapasua anga.

Hapa Spoti Xtra linakuletea namna wababe hao wanavyopambana kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa hatua ya makundi ambapo Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga Kombe la Shirikisho Afrika.

USHAMBULIAJI

Yanga kwenye dakika 270, imekuwa ni moto anga hizi hatua ya makundi ambapo wametupia mabao manne, kila nyota ana bao mojamoja.

Mtupiaji wa kwanza alikuwa Kennedy Musonda kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe, kisha Mudhathir Yahya na Tuisila Kisinda ambao nao walifunga wakati Yanga ikishinda 3-1 dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Bao moja ni mali ya Fiston Mayele ambaye alifunga kwenye mchezo dhidi ya Real Bamako ugenini kwenye sare ya kufungana bao 1-1

Simba kwenye mechi tatu kimataifa ambazo ni dakika 270, bao moja wamefunga, huku mtupiaji akiwa ni Henock Inonga ambaye ni beki, ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Vipers ugenini.

Kikosi cha Simba

ULINZI

Hapa Yanga imeokota mabao manne nyavuni kwenye mchezo wa kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya US Monastri ugenini, wa pili walishinda mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe na ule wa tatu ngoma ilikuwa Real Bamako 1-1 Yanga. Kwenye kila mchezo wametunguliwa.

Simba kwenye ulinzi walianza kutunguliwa dhidi ya Horoya bao 1-0, wakachapwa na Raja Casablanca 0-3 Uwanja wa Mkapa, kisha dhidi ya Vipers hawakutunguliwa, walishinda bao 0-1.

Yanga na Simba kila moja imetunguliwa mabao manne kwenye mechi za kimataifa hatua ya makundi.

MANULA NA DIARRA

Aishi Manula ambaye ni kipa wa Simba, anapata tabu akiwa amepata kazi ya kupigiwa penalti mbili, huku moja akiipangua dhidi ya Horoya na dhidi ya Raja Casablanca alitunguliwa. Kwenye mechi tatu hajafungwa mechi moja, ilikuwa dhidi ya Vipers.

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra, kwenye mechi tatu katunguliwa kila mechi akiwa hajakusanya clean sheet yoyote.

MABEKI

Beki wa Simba, Henock Inonga ni yeye mwenye bao kimataifa huku Joash Onyango akiwa amesababisha penalti mbili, dhidi ya Horoya na Raja Casablanca.

WAKALI WA PASI

Aziz KI ana pasi moja ya bao dhidi ya Real Bamako, alimpa Mayele ambaye naye ana pasi moja ya bao dhidi ya TP Mazembe, alimpa Tuisila Kisinda.

Kenedy Musonda ana pasi moja ya bao, alimpa Mudhathir Yahya, bao la Musonda alitumia pasi ya Djuma Shaban.

Kwa Simba ni Moses Phiri alimpa pasi ya bao Inonga dhidi ya Vipers.

MIPIRA YA KUTENGWA TATIZO

Yanga mabao yake yote manne yametokana na mapigo huru huku Simba ikitunguliwa bao moja kwa penalti.

YANGA

Kwenye Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ipo nafasi ya pili, ina pointi nne baada ya kucheza mechi tatu, imeshinda moja, sare moja, imetunguliwa mechi moja. Tofauti yao na vinara ambao ni US Monastri ni pointi tatu ambapo wao wamekusanya pointi saba.

Wanaoburuza mkia ni Real Bamako, wana pointi mbili, wamepoteza mchezo mmoja, kisha sare mbili, huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa TP Mazembe, ina pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu, imeshinda mchezo mmoja, ikiwa imepoteza mechi mbili.

SIMBA

Kwenye Kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi tatu, imepoza mechi mbili, ikiwa imeshinda mchezo mmoja.

Raja ni wababe wa kundi wakiwa wamekusanya pointi 9 baada ya kucheza mechi tatu na kushinda zote, wakitupia mabao 10.

Vipers wanaburuza mkia wakiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu, hawajaambulia ushindi huku wakiwa wamepata sare moja na kutunguliwa mechi mbili.

KUNDI D KOMBE LA SHIRIKISHO

P       W     D       L        GF    GA    GD    Pts

  1. US Monastir 3 2       1       0       5       1       +4     7
  2. Yanga 3 1       1       1       4       4       0       4
  3. TP Mazembe 3 1       0       2       4       6       −2     3
  4. Real Bamako 3 0       2       1       3       5       −2     2

 

MATOKEO & RATIBA YA YANGA

FEBRUARI 12, 2023

US Monastir     2–0  Yanga

FEBRUARI 19, 2023

Yanga       3–1  TP Mazembe

FEBRUARI 26, 2023

Real Bamako   1–1  Yanga

MACHI 8, 2023

Yanga       v       Real Bamako

MACHI 19, 2023

Yanga       v       US Monastir

 

APRILI 2, 2023

TP Mazembe   v       Yanga

 

KUNDI C LIGI YA MABINGWA

P       W     D       L        GF    GA    GD    Pts

  1. Raja CA 3 3       0       0       10     0       +10  9
  2. Horoya 3 1       1       1       1       2       −1     4
  3. Simba 3 1       0       2       1       4       −3     3
  4. Vipers 3 0       1       2       0       6       −6     1

 

MATOKEO & RATIBA YA SIMBA

FEBRUARI 11, 2023

Horoya     1–0  Simba

 

FEBRUARI 18, 2023

Simba       0–3  Raja CA

 

FEBRUARI 25, 2023

Vipers       0–1  Simba

MACHI 7, 2023

Simba       v       Vipers

MACHI 18, 2023

Simba       v       Horoya

 

MACHI 31 – APRILI 1, 2023

Raja CA    v       Simba

MAKALA  NA LUNYAMADZO MLYUKA

NAMNA MPYA ya USHANGILIAJI kwa WANANCHI, WANANCHI JOGGING KUKIWASHA JUMAPILI…..

Leave A Reply