The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Zawakutanisha Lowassa, Nape na Ridhiwani

Ridhiwani Kikwete, (Kulia) akimpa mkono mmoja wa mwanadama wa chama wa Chadema baada ya kumsalimia Edward Lowassa

MECHI ya jana ya watani Simba na Yanga ambapo Simba iliichapa Yanga mabao 2-1 iliwakutanisha viongozi wa ngazi za juu nchini wakiwemo Edward Lowassa, Nape Nauye na Ridhiwa Kikwete katika Uwanja wa Taifa ambapo waliweka pembeni itikadi zao za vyama.


Lilikuwa ni tukio la aina yake uwanjani baada ya Ridhiwan akiwa ni shabiki wa kutupwa wa Yanga na Lowassa akiwa Simba, walikutana na kupeana salamu kama watani wa jadi.

Magoli ya Simba yalifungwa na Laudit Mavugo na Shiza Kichuya ambapo la Yanga lilifungwa kwa penalti na Simon Msuva.

 

 

Na Salum Milongo/GPL

Comments are closed.