The House of Favourite Newspapers

Simba Yapigwa na JKT Tanzania Bao 1-0, Adam Adam Apeleka Kilio Simba

0

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na JKT Tanzania umekamilikwa kwa Simba kubanwa mbavu kwa kufungwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Adam Adam dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza ambalo limedumu mpaka mwisho wa kipindi.

Nyota wapya wa Simba, Luis na Shiza Kichuya wameanza leo kwa mara ya kwanza.

Mashabiki wamejitokeza kushuhudia ushindani uliopo kwani leo ni mechi ya kisasi.

Mchezo wa kwanza walipokutana Simba ilishinda mabao 3-1 na leo kisasi kimelipwa kwa JKT kushinda bao 1-0.

Leave A Reply