Simba Yasitisha Mkataba wa Ibrahim Ajibu – Video

 

UONGOZI wa Klabu ya Simba umethibitisha kusitisha mkataba wa kiungo fundi Ibrahim Ajibu. Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Simba imeeleza kuwa imefikia makubaliano ya pande zote mbili kwa maslahi mapana kusitisha mkataba wa kiungo huyo mshambuliaji.

 

“Kwa maslahi ya pande zote mbili, uongozi wa klabu umefikia makubaliano na mchezaji Ibrahim Ajibu kusitisha mkataba wake kuanzia leo Alhamisi Desemba 30, 2021.

Kipekee tunamshukuru Ajibu kwa namna alivyojitoa kupambana kwa ajili ya Simba, na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake.”  wamesema Simba SC

 

Ajibu alirejea nyumbani kwa mara nyingine tena akitokea Yanga ambapo alipokuwa huko alikuwa ni nahodha na alipofika Simba mambo yalikuwa magumu kwake.

 

Jana Desemba 29 wakati wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi Uwanja wa Bunju Complex kujiaandaa na mchezo ujao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Januari Mosi 2022 Uwanja wa Mkapa hakuwepo mazoezini.702
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment