The House of Favourite Newspapers

SportPesa Waiongezea Mkataba Namungo FC

0

KAMPUNI ya michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania, imeongeza mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini timu ya Namungo ya Ruangwa, Lindi.

 

SportPesa imeingia makubaliano hayoya kuendelea na udhamini Namungo baada ya pande mbili zote kufikia muafaka mzuri wa kuongeza mkataba.

 

Namungo ni kati ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambayo hivi sasa ipo katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 13 ikicheza michezo kumi pekee.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kuwa wana furaha kubwa kufikia makubaliano mazuri ya kuendelea na udhamini Namungo.

 

Tarimba alisema kuwa mkataba wa mwaka mmoja wameingia na Namungo baada ya ule wa awali ukitarajiwa kumalizika mapema Januari, 2022.

 

“Tunafuraha kubwa kufikia makubaliano mazuri na Namungo baada ya kufanya mazungumzo yaliyotushawishi kuendelea na udhamini timu ya Namungo”.

“Tunaamini kwa kupitia udhamini huu tulioutoa Namungo utasaidia katika masuala ya maendeleo katika timu hiyo inayoshiriki ligiKuuya NBC”.

 

“Kama SportPesa tutaendelea kuunga mkono mchezo wa soka kwa kupitia udhamini ambao tunaoutoa kutoka katika klabu mbalimbali zikiwemo klabu kubwa za Simba na Yanga,”alisema Tarimba.

 

Kwa upande wa Namungo, Mtendaji Mkuu (C.EO) wa timu hiyo, Omary Kaya alisema kuwa “Tunaishukuru SportPesa kwa udhamini ambao imekuwa ikitupatia tangu ilipoanza kutudhamini”.

 

“Hivyo tutaendelea kufanyakazi pamoja na SportPesa kwa kutimiza masharti ya kimkataba ikiwemo kuwatangaza vizuri”.

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza SportPesa kwa juhudi kubwa wanazoendelea katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua kupitia udhamini wanaoutoa,”alisema Kaya

Leave A Reply