The House of Favourite Newspapers

Simba Yatishia Afrika Kuvaana USGN, Niger

0

KUELEKEA michezo yao miwili ya ugenini ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa umekamilisha maandalizi yote muhimu ya michezo hiyo, huku wakitamba kuwa wanataka kuvuna pointi zote sita za ugenini.


Simba inakwenda kwenye
michezo hiyo ikiwa imeweka rekodi ya kufunga mabao 10 katika michezo miwili iliyopita jijini Dar es Salaam – ushindi wa 3-1 dhidi ya Asec Mimosas kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, na ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


Kiwango walichokionyesha
kwenye mechi hizo mbili, kimetosha kuwaaminisha mashabiki wao kuwa Simba imerejea kwenye makali yake, na sasa wanaamini kikosi chao hakikamatiki.


Simba ambayo imepangwa kundi
D la michuano ya kimataifa ya Shirikisho, inatarajiwa  kuvaana na USGNkeshokutwa Jumapili nchini Niger, kabla ya kucheza dhidi ya RS Berkane nchini Morocco Februari 27.

 

Kuelekea michezo hiyo, tayari maafisa wa Simba wameshawasili nchini Niger kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya sehemu ambayo timu inayoondoka leo itafikia na kujifua kuelekea mchezo huo.


Akizungumza na Championi
Ijumaa, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema: “Kwanza kama sehemu ya uongozi wa Simba napenda kuwapongeza wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa ujumla kwa ushindi mnono dhidi ya Ruvu Shooting.


“Ushindi huo umezidi kutupa ari
ya kufanya vizuri kuelekea michezo yetu miwili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN na RS Berkane ambayo kama uongozi tumefanya maandalizi yote kuhakikisha tunapata pointi zote sita ugenini, kabla ya kurejea tena kujipanga kwa ajili ya michezo miwili ya nyumbani, tunaamini kutokana na maandalizi tuliyoyafanya tutafanikiwa.”

 

Naye Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka leo saa 11:00 jioni kuelekea nchini Niger kwa ajili ya mchezo huo.

 

Kikosi hicho kinaondoka na wachezaji 23, akiwemo Clatous Chama ambaye amepewa kazi maalum, kwa kuwa hatacheza kutokana na kanuni kumbana (aliichezea Berkane katika michuano hii).

 

“Kikosi chetu cha Simba kinatarajiwa kuondoka na wachezaji 23 akiwemo Chama, ambaye licha ya kutokuwa sehemu ya mechi, lakini ana kazi maalumu ya kuisaidia timu hiyo.


“Hatuna hofu, uzuri tayari
tulituma watu kwenda Niger kufanya uchunguzi na tayari wamekamilisha suala la usafiri, sehemu ya kufikia na chakula.


“Na mara baada ya kumaliza
mchezo wetu huko Niger hatutarudi nchini na badala yake tunaunganisha Morocco kwenye mechi dhidi ya Berkane,” alisema Ally.

 

Wachezaji wanaotarajiwa kusafiri na timu hiyo ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salum, Shomari Kapombe,Israel Mwenda, Jimmyson Mwanuke, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael, Joash Onyango, Pascal Wawa na Henock Inonga.


Wengine ni Kennedy Juma, Erasto
Nyoni, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Ousmane Sakho,
Peter Banda, Bernard Morrison, John
Bocco, Meddie Kagere, Yusuph Mhilu na Clatous Chama.


Wachezaji watakaobaki ni watano
ambao ni Larry Bwalya, Cris Mugalu, Denis Kibu, Hassan Dilunga na
Taddeo Lwanga walio na majeraha
huku Bwalya akiachwa kutokana na kupatwa na msiba.

Leave A Reply