The House of Favourite Newspapers

Lulu: Wala Hata Siwacheki

0

ELIZABETH Michael almaarufu Lulu ametoka mbali mno na tasnia ya Bongo Movies tangu akiwa na umri wa miaka mitano hadi sasa ni mke na mama wa mtoto mmoja ambaye anasema kuwa, hawezi kuwacheka mastaa ambao wanakwenda kufanya sajari mbalimbali kwa sababu kila mtu anafanya kitu anachokipenda kwenye maisha yake.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Lulu anasema kuwa, watu wengi wanawasema watu ambao wanakwenda nje ya nchi.lakini yeye haoni kama kuna tatizo kwa sababu nafsi zao zimeridhia kila kitu.

 

“Mimi wala hata siwacheki watu ambao wameenda kufanya sajari kwa sababu ndicho kitu ambacho kinawavutia na akili zao zinawaambia wazi watapendeza na wanafurahia wanachokifanya, hilo ndilo la msingi kabisa,” anasema Lulu mara baada ya kufungua duka lake lingine la nguo maeneo ya Sinza jijini Dar.

 

Lulu anasema kuwa, kwa upande wake anasema kuwa, hajaona kitu chochote kwenye mwili wake cha kukiongeza au kukipunguza.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply