The House of Favourite Newspapers

Simba Yatoa Kipigo cha 5G kwa Mtibwa Sugar

0

MABINGWA wa Watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba, wamerudi kwa kishindo kwenye ligi hiyo baada ya kuicharaza Mtibwa Sugar kwa magoli 5-0 katika mchezo uliochezwa leo Aprili 14,   kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

 

Magoli ya Simba yamefungwa na Claoutus Chama dakika ya 9’ Rally Bwalya dakika 19’ Meddie Kagere alifunga magoli mawili 42’ 51’ na Luis Miquissone aliyehitimisha karamu hiyo akimalizia pasi safi ya Chama dakika ya 69.

Kagere baada ya kupachika mabao wawili amefikisha magoli 11,   na kuongoza msimamo ya wafungaji kwenye ligi kuu bara.

 

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 49 baada ya kuchexa mechi 21 na kusogea mpaka nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga wenye alama 51 baada ya kushuka dimbani mara 24.

Leave A Reply