The House of Favourite Newspapers

Simbu Ashika Nafasi Ya Tatu, Abeba Medali Ya Shaba London

0

 

Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Simbu.

MWANARIADHA Mtanzania, Alphonce Simbu, jana alifanikiwa kubeba medali ya shaba kwenye mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea jijini London, England baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio za marathon.

Simbu ameshika nafasi ya tatu baada ya kukimbia kwa muda wa 02:09:51, huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Mkenya, Geofrey Kirui aliyekimbia kwa 02:08:27 na Muethiopia, Tamirat Tola (02:09:49).

Kwa kushika nafasi hiyo ya tatu, Simbu atajinyakulia kitita cha dolla 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22 za Kitanzania).

Leave A Reply