The House of Favourite Newspapers

Simbu Awashukuru Watanzania, Nape Atoa Neno

simbu-nape-7 Waziri Nape Nnauye akizungumza na wadau na wanahabari wakati wa hafla ya kumpokea mwanariadha Simbu.

KINARA wa Standard Chartered Mumbai Marathon ambaye ni balozi maalum wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Alphonce Felix Simbu, amewashukuru Watanzania kwa kuendelea kumsapoti na amewaomba kwa pamoja washirikiane kuitangaza nchi kimataifa.

simbu-nape-6Simbu akitoa neno la shukrani.

Simbu ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kumpongeza iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

simbu-nape-2

Kinara wa Standard Chartered Mumbai Marathon ambaye ni balozi maalum wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Alphonce Felix Simbu (kulia) akimkabidhi tuzo yake

Hafla hiyo imekuja baada ya Jumapili wiki iliyopita Simbu kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mbio za Mumbai Marathon zilizofanyika India na kuwabwaga Wakenya na Waethiopia walioshika nafasi ya pili mpaka kumi.

simbu-nape-1Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa na tuzo ya Simbu.

“Kama mlifuatilia zile mbio, katika kumi bora, kulikuwa na Wakenya saba na Waethiopia wawili, huku Mtanzania nikiwa peke yangu, kama nisingejitahidi basi Tanzania tusingekuwa na furaha kama hii.

simbu-nape-3

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo akiwa na tuzo ya mwanariadha huyo.

“Hivyo niombe tu tushirikiane wakati mwingine tuandae wanariadha wengi ili kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, naamini tukifanya hivyo nchi yetu itakuwa juu ndani ya kipindi kifupi,” alisema Simbu.

simbu-nape-4Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alimpongeza shujaa  Simbu kwa ushindi huo na Kampuni ya Multichoice kwa kuitangaza nchi kimataifa.

simbu-nape-5“Serikali peke yake haiwezi kufanikisha hili, hivyo nitoe wito kwa makampuni binafsi kuja kwetu tushirikiane kuwekeza katika vipaji kama hivi, tunataka siku zijazo tuwe na mashujaa wengi kama Simbu, isiwe tu kwenye michezo, bali hata katika muziki na sanaa mbalimbali, naamini dunia itatutambua vilivyo,” alisema Nape.

simbu-nape-8Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, alisema wataendelea kumdhamini Simbu, na wanataka awe chachu na hamasa kwa vijana wanaochipukia ili waone kweli kila kitu kinawezekana akisisitiza kwamba kikubwa ni kujituma tu.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.