The House of Favourite Newspapers

Kongamano la Wajasiliamali Wanawake Simiyu, NBC Wamkosha Bashungwa

0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa akizungumza na wanawake wajasiriamali zaidi ya 400 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ambao walishiriki kwenye Kongamano la Biashara na Kilimo lililoandaliwa na Jumuiya wa Wafanyabiashara wanawake na Vijana (TABWA), kwa kushirikiana na Benki ya NBC na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). Kongamano hilo linafanyika kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

 

Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje akizungumza na wanawake wajasiliamali zaidi ya 400 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ambao walishiriki kwenye Kongamano la Biashara na Kilimo lililoandaliwa na Jumuiya wa Wafanyabiashara wanawake na Vijana (TABWA) kwa kushirikiana na Benki ys NBC na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) linalofanyika kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Kulia) akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Jumuiya wa Wafanyabiashara wanawake na Vijana (TABWA), Doreen Mawala ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Waziri huyo katika kuwasaida wajasiliamali wananawake nchini.

 

Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo.

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Kulia) akimsikiliza Verimund Kapinga (Kushoto) kutoka kampuni ya ETC Agro ambayo ni mteja wa Benki ya NBC na mdau wa Kilimo wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu. Anaeshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Katikati).

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Kulia) akizungumza na mmoja wa wajasiliamali ambae mteja wa Benki ya NBC Melina Cheisa (Kushoto) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu. Anaeshuhudia ni Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje (katikati).

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Katikati) akizungumza na Bi Teddy Mosha (Kulia) kutoka kampuni ya uzalishaji wa mafuta ya alizeti ya Gilitu Enterprises ambae ni mteja wa benki ya NBC wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu. Anaeshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (alievaa Tshirt nyeupe).

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Kulia) akizungumza na Hekela Sigalla (Kulia) kutoka kampuni ya utengenezaji wa mashine za samani (furniture) ya Azienda Group ambae ni mteja wa benki ya NBC wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu. Anaeshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (kushoto).

 

Leave A Reply