The House of Favourite Newspapers

Samatta: Alikiba Usinifokee

0

NAHODHA wa timu ya taifa ya soka nchini (Taifa Stars) na mchezaji wa Klabu ya Aston Villa ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) Mbwana Samatta, amemtaka msanii Alikiba ‘asimfokee‘ na kumtambia kuelekea kwenye mchezo wa SamaKiba utakaochezwa siku ya August 8, 2020, Uwanja wa Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Samatta amesema amejipanga kwa ushindi kwa mara ya tatu mfululizo na mapato yatakayopatikana katika mchezo huo yatapelekwa kwenye Wizara ya Elimu ili kushughulikia changamoyo ya masuala ya elimu hapa nchini.

 

“Timu yangu ya ushindi kama kawaida nimejiandaa kushinda kama michezo miwili iliyopita, naona figisu za marefa zimeanza lakini nina uhakika nitashinda tena kwa mara ya tatu mfululizo kwa sababu sijaona kizuizi.  Mimi nimemaliza maana Alikiba kaongea saa mbili, Haji Manara naye kaongea saa nne, na Alikiba usinifokee kabisa nitakuchapa hata ufanye nini,” amesema Mbwana Samatta

 

Team Samatta amegusia timu yake itakuwa na wachezaji kama Kagere na Yondani na msemaji wake ni Haji Manara, huku Team Kiba itakuwa na wachezaji kama Ibrahim Ajib, Abdu Kiba na msemaji wake ni Official Mwalubadu.

 

Manara

“Safari hii nitakuwa na jukumu la kusemea timu zote mbili kwa sababu msemaji wa Alikiba, Mwalubadu amepigwa pini Norway, Team Samatta itakuwa na watu kama Kaseja, Yondani na Kagere na Team Kiba watakuwepo akina Ajibu na Mwamnyeto na wengineo,”  alisema Manara.

Leave A Reply