The House of Favourite Newspapers

Singida Big Stars, Yanga Kinawaka Leo Nusu Fainali Azam Sports Federation Cup

0

BENCHI la Ufundi la Singida Big Stars, limeweka wazi kuwa lipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa nusu fainali Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga.

Timu hiyo inayonolewana Kocha Mkuu, Hans van Der Pluijm, inapambana na mabingwa watetezi wa taji hilo, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Pluijm amesema wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo na wataingia kwa tahadhari kupata ushindi ili watinge hatua ya fainali.

“Wapinzani wetu tunatambua ni timu bora na kila timu inahitaji ushindi, hivyo tutaingia kwa tahadhari kutafuta ushindi, tulipata muda wa kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huu,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.

Cedric Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga raia wa Burundi, amesema wanatambua uimara wa wapinzani wao, hivyo wataingia uwanjani kwa tahadhari kupata ushindi.

“Kila mchezaji anatambua uimara wa wapinzani wetu, licha ya ratiba kuwa ngumu, haiwezi kuwa sababu ya kupoteza, tutaingia kwa hesabu za kusaka ushindi,” alisema Kaze.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply