The House of Favourite Newspapers

Singida Yampa Mkataba Ndugu wa Niyonzima

0
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima.

Said Ally na Musa Mateja, Championi Jumatano, Habari

KUONYESHA kwamba wamepania kufanya vyema kwenye msimu ujao wa ligi kuu, uongozi wa kikosi cha Singida United, upo mbioni kumleta kiraka wa Polisi Rwanda, Dan Usengimana raia wa nchi hiyo, anayotokea kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

Mpaka sasa Singida United inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans Pluijm imeshamalizana na nyota kadhaa wa kimataifa wakiwemo Wazimbabwe, Tafadizwa Kutinyu, Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa pamoja na Mganda, Shafik Batambuze. Kocha msaidizi wa Singida, Fred Felix Minziro ameliambia Championi Jumatano, kuwa wanaendelea kufanya usajili kwa ajili ya kukifanya kikosi chao kiweze kupambana na timu kubwa za Simba na Yanga kwenye msimu ujao wa ligi.

“Wikiendi hii tutamleta mchezaji mpya kutoka Rwanda ambaye anaichezea timu ya Polisi ya nchini humo, Dan Usengimana kwa ajili ya kujiunga na sisi baada ya kufikia makubaliano baina ya pande mbili. “Tumeamua kusajili wachezaji walio kwenye viwango vikubwa kwa sababu tunataka kushindana na timu kubwa kwenye ligi na lengo letu ni kuhakikisha tunatingisha kwenye ligi na kushika nafasi za juu,”alisema Minziro.

Leave A Reply