The House of Favourite Newspapers

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka

0

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, niliwahi kuishi mkoani Geita kwenye machimbo ya dhahabu yaitwayo Mugusu, waliokuwepo maeneo hayo wakati huo watakumbuka, palitokea mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na kutapita, baadaye ukathibitika kwamba ni kipindupindu.Watu wengi sana walipoteza maisha na wengi walikimbia kurejea makwao, jambo moja lililonishangaza na kunifanya niamini kuna uhusiano mkubwa sana kati ya hofu na kinga ya mwili dhidi ya magonjwa, ni kwamba; mwendawazimu mmoja aliyekuwa akiishi pale mgodini na kula majalalani, hakuugua kipindupindu wala kufa.

 

Waliopoteza uhai, wengi walikuwa ni watu wenye akili zao timamu!Mwaka 2017, akiwakilisha mada yake yenye kichwa cha habari Physiology of Fear and Its Impact on Wellness (Hofu na Madhara Yake Kwenye Afya ya Binadamu) kwenye mkutano wa wataalam wa sayansi na ubongo na mishipa ya fahamu (Neuroscience Education Institute Congress), uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Pacific Lutheran University huko Marekani, Dk Mary D.

Moller (PhD) alisema; “Hofu ni hisia ya ndani ya akili ya mwanadamu, hutokea pale ambapo mfumo wa hisia katika ubongo unapogundua kwamba kuna kitu nje ya mwili kinachosababisha utisho au hatari.”Aliainisha hatua tatu muhimu ambazo hutokea pale mwanadamu anapokumbwa na hofu, hatua hizo ni;

  • TAHADHARI –Hii ni hatua ya mwanzo kabisa ambapo mfumo wa akili wa mwanadamu hugundua kuna hatari na hujiandaa kukabiliana nayo kwa kutengeneza viamsho (hormones) kama cortisol, adrenaline na nor-adrenaline, viamsho hivi huuwezesha mwili wa mwanadamu kukabiliana ama kuepuka hatari.
  • MAREKEBISHO –Hii huitwa pia ‘resistance stage’ ambayo hufuata baada ya mwili kukabiliana na hatari, viamsho vya mwili (hormones) zilizokuwa zimepanda, hurejea katika hali yake ya kawaida na pia mwili hujifanyia marekebisho kama kuna madhara yaliyokuwa yametokea.
  • KUCHOKA –Hii pia huitwa ‘exhaustion stage’ hutokea pale ambapo hofu imedumu kwa muda mrefu kiasi kwamba, uwezo wa mwili kukabiliana na hofu hupungua sababu unakuwa umepoteza nguvu nyingi sana kukabiliana na msongo ama hofu yenyewe.Dk Moller alifafanua zaidi hatua hii ya tatu kuwa ndiyo huleta matatizo makubwa katika mwili wa mwanadamu, kwani hofu ikidumu kwa muda mrefu, husababisha madhara kimwili hasa katika maeneo matatu; kinga ya mwili, mfumo wa kutengeneza viamsho (endocrine system) na mfumo wa mishipa ya fahamu (autonomic nervous system). Mambo haya ndiyo humfanya binadamu mwenye hofu apoteze kinga ya mwili dhidi ya kupambana na maradhi

Alichokisema Dk Moller, ndicho kilimfanya mwendawazimu kule Mugusu asiugue kipindupindu wakati watu wenye akili zao timamu walikuwa wakifa, kwa kutoelewa kilichokuwa kinaendelea, mwendawazimu hakuwa na hofu yoyote, kinga yake iliendelea kubaki imara na waliokuwa na hofu nyingi, walishusha kinga zao na kujikuta wakiugua.

 

Hiki ndicho kinachoendelea duniani kwa sasa, watu fulani wameamua kuwatia wanadamu hofu, waogope Virusi vya Corona kuliko ugonjwa mwingine wowote! Wanadamu tunajazwa hofu kutoka kila kona, ukifungua redio ni Virusi vya Corona, ukienda kwenye runinga ni Virusi vya Corona, ukisoma gazeti ni Virusi vya Corona, mtandaoni hivyohivyo habari ni moja Virusi vya Corona vinaua.

 

Sikatai ugonjwa huu mpya ni hatari na unaua, lakini naamini hauui kama inavyoua malaria, Saratani au ajali za barabarani, mambo ambayo hayaongelewi sana kama inavyotokea kwa Ugonjwa wa COVID-19 unaopewa nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari na kuwajaza watu hofu.Nini lengo la kampeni hii ya kuwajaza watu hofu? Mimi naamini na ninafikiri hata Rais DK John Pombe Magufuli anaamini hivyo, kwamba kinacholengwa hapa ni kinga zetu za mwili, zinataka kuporomoshwa pale tutakapokuwa na hofu nyingi mioyoni mwetu.

Kama inafika mahali huko Ulaya madaktari wanalipwa fedha ili kila mgonjwa anayekufa aandikiwe amekufa kwa Corona kuonesha kwamba ugonjwa huu unaua watu wengi, kuna watu wamedhamiria kutujaza hofu ili kinga zetu zipungue na baadaye tuambukizwe.

 

Vipimo vya Corona vinatoa majibu ya uongo, kuonyesha kwamba watu wengi wameambukizwa ili binadamu tuzidi kutishika na kuogopa zaidi na kwa sababu kuna uhusiano kati ya hofu na kinga ya mwili, basi kinga zetu zitashuka na itakuwa rahisi kwetu kuambukizwa, lengo ni nini? Kuna watu nyuma ya mpango huu, wanaotaka kutengeneza mabilioni ya Dola kwa kuwachanja watu dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19.

 

Rais John Magufuli akiwa ni mwanasayansi aliyebobea, aliligundua jambo hili tangu mapema, akaanza kuhisi kwamba kulikuwa na uwezekano hata vifaa vya kupimia Corona au barakoa kutoka nje kuwekewa vidudu vya ugonjwa huu ili watu waugue, akaamua jambo moja tu kupambana na hofu na kuingiza moyo wa ujasiri ndani ya watu wake ili kinga zao zisiporomoke, akijua kabisa ya kwamba mtu mwenye kinga imara asingeugua ugonjwa huo.

“Haka kaugonjwa ka Corona, katapita kama magonjwa mengine yaliyopita, cha muhimu tuendelee kumuabudu Mungu wetu,” mara kadhaa amesikika akisema maneno hayo, lengo lake likiwa ni kuondoa hofu katika mioyo ya watu wake na kuwajengea imani ya kupata ushindi, hili ndilo limefanya Watanzania wengi wasife kwa ugonjwa huu kama ilivyotegemewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).Siri kubwa ya ushindi huu ni kupambana na hofu, pamoja na kuimarisha kinga zetu za mwili kwa kula vyakula vyenye Vitamin C na Zinc ya kutosha.

Yeyote atakayeyafanya haya, akaongezea na kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya hata kama atakuwa hajajifungia ndani (lockdown), bado ataibuka mshindi dhidi ya Corona.Ni lazima tuelewe uhusiano uliopo kati ya hofu na kinga ya mwili dhidi ya magonjwa, hofu nyingi kinga dhaifu; ukosefu wa hofu kinga imara ya mwili dhidi ya magonjwa, mimi naamini Wamarekani pamoja na mambo mengine, wanakufa sana kwa Corona kutokana na hofu waliyojazwa mioyoni mwao na vyombo vya habari, kiukweli, nionavyo mimi haipo hata sababu ya kuendelea kutangaziana kila siku leo wamekufa wangapi, wameambukizwa wangapi, kwa sababu haya ndiyo yanayotujaza hofu na kushusha kinga zetu za mwili na hatimaye tunaambukizwa Corona na kufa.

Leave A Reply