The House of Favourite Newspapers

SKENDO YA KUKODI WATUKANAJI MTANDAONI WASTARA, ESMA WATOA POVU!

Image result for wastara juma
Wastara Juma

BAADA ya hivi karibuni dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan na msanii wa filamu, Wastara Juma kuporomosha matusi mazito mtandaoni baada ya kutibuliwa, skendo iliyoibuka ni kwamba, mastaa hao walikodi watu wa kuwasaidia kutukana kwani wao hawana umahiri huo.  Mmoja wa watu wa karibu wa Esma alilitonya gazeti hili kuwa, kwa anavyomfahamu mwanadada huyo hana uwezo wa kuporomosha matusi yale ila anachojua ni kwamba, kuna mtu alimlipa ili amsaidie kutukana.

“Mimi namjua vizuri Esma, hana uwezo na ujasiri wa kutukana vile, kuna dada mmoja anaitwa Fatuma Mcharuko wa Kinondoni, yule kazi yake ni kukodiwa ili awachambe watu kwenye mitandao, nahisi na yeye kamkodi. “Halafu unajua Wastara na Esma lao moja, usije ukashangaa kusikia pia kuwa Fatuma kalipwa ili awaandikie wote kwenye kurasa zao matusi kisha kuposti. Ila jamani haya mambo sijui yatakoma lini, unapotukana vile matusi ya nguoni si ni kama unajitukana na kujidhalilisha mwenyewe? Sisi yetu macho,” alisema sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.Image result for esma platnumz

Kufuatia madai hayo ya mastaa hao kusaidiwa kuandikiwa matusi kwenye kurasa zao za Instagram kisha kulipa pesa, gazeti hili lilifanya jitihada za kuwatafuta ambapo walipopatikana kwa nyakati tofauti walitoa povu si la nchi hii. ““Kwa nini nitume mtu anisaidie kutukana na wakati mimi mwenyewe naweza kufanya hivyo? Mtu akinitibua najua kabisa watu wengi sana watakuwa wananishangaa sana kwenye hiyo ishu kutokana na nilivyokuwa nikiandika lakini imenibidi kufanya hivyo na wala hakuna mtu aliyeniandikia mimi,” alisema Wastara.

Naye Esma akafunguka hivi: “Kwa nini niandikiwe na wakati mimi mwenyewe naweza kutumia mikono yangu na uzuri simu yangu ipo vizuri tu kufanya kazi hiyo. Halafu inatokea tu mtu unajikuta umeingia kwenye matusi kutokana na mtu alivyokutukana na mimi kawaida yangu nitamheshimu atakayeniheshimu tu.”

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi

Comments are closed.