The House of Favourite Newspapers

Smirnoff Ice Black Yarudi Sokoni kwa Kishindo

0
Baadhi ya wateja wa kinywaji cha Smirnoff Ice wakifurahia kinywaji hicho baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kukirudisha tena sokoni baada ya kutopatikana kwa muda. Hafla ya kutangaza kukirudisha sokoni kinywaji hicho ilifanyika jijini Dar jana. 

 

WATUMIAJI wa kinywaji cha Smirnoff Ice Black wana kila sababu ya kufurahi baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kukirudisha sokoni kinywaji hicho baada ya kukosekana kwa muda.

 

Smirnoff Ice Black ni kinywaji kilichochanganywa na kilichopo tayari kwa ajili ya kutumiwa ambacho ni sehemu ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni mama ya SBL, Diageo.

 

Wacheza muziki wa kikundi cha DWC dance cha jijini Dar es Salaam, wakitoa burudani safi kwa watumiaji wa kinywaji cha Smirnoff Ice waliojitokeza wakati wa halfa ya Kampuniya Bia ya Serengeti kutangaza kukirudisa tena sokoni kinywaji hicho.

 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam, meneja uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus alisema kinywaji hicho sasa kitakuwa kinapatikana kila sehemu na kuwataka watumiaji wake kuendelea kukifurahia.

 

 

“Baada ya kusubiri kwa muda, sasa tumewaletea tena kinywaji hiki cha kimataifa ili muweze kuendelea kukifurahia,  Ni kinywaji chenye ladha nzuri na ya kipekee ambayo unaweza kuifurahia na marafiki,” alisema.

 

DJ Bafa mmoja kati wa washindi wa kipindi cha nyuma wa shindalo la kusaka Ma-DJ lilikuwa linaendashwa na kinywaji cha Smirnoff akitoa burudani ya kupiga muziki wakati wa halfa kutangaza kurudi sokoni kwa kinywaji cha Smirnoff iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

 

 

 

Bertha alisema pamoja na kuwaburudisha watumiaji wake, Smirnoff Ice Black imekuwa ikiunga mkono jitihada za kuendeleza vipaji mbali mbali vya vijana ikiwa ni pamoja na shindano la kusaka vipaji vya Ma-DJ wachanga ambapo tayari limeshafanyika mara tatu kipindi cha Nyuma.

 

“Kikiwa pia ni kinywaji kinachounga mkono ukuzaji wa vipaji, baada ya kurudi sokoni tutakwenda mbali zaidi kwa kuunga mkono siyo tu kutafuta Ma-DJ bali hata vipaji vingine  na kwa hiyo vijana wa Kitanzania waendelee kufuatilia kwa ukaribu ili waweze kusikia na kupata fursa kutoka Smirnoff Ice Black,” alisema.

Leave A Reply