The House of Favourite Newspapers

SMZ Kugharamia Mazishi ya Walioangukiwa na Jumba la Maajabu

0

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeahidi kugharamia mazishi ya watu wawili waliofariki baada ya kudondokewa na jengo maarufu la kitalii, Beit Al Ajaib (Jumba la Maajabu) lili-lopo eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja visiwani humo.

 

Waliofariki ni Pande Haji Makame (39) na Burhani Ameir Makuno (34) walibainika kati ya saa sita na saa nane usiku kwenye jitihada za kuwatafuta waliofunikwa na kifusi cha jen-go hilo.

 

Wakati wawili hao wakitolewa katika kifusi, wengine wanne walikuwa wakitib iwa majereha waliyoyapata katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

 

Jumba hilo maarufu lililodumu kwa zaidi ya miaka 130 lilidondoka juzi mchana na kuwafunika mafundi waliokuwa wakilikarabati jana Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla akifuatana na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya aliwatembelea majeruhi waliolazwa na kwenda eneo la tukio.

 

Naibu kamishna wa kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar, kamanda Gora Haji Gora alimweleza Abdulla kwamba uokoaji kufanyika kwa tahadhari kubwa kutokana na mazingira ya tukio lilivyokuwa.

 

Kamanda Gora alisema operesheni ya kuondoa kifusi cha jengo hilo itaendelea ili kubaini kama kuna watu wengine waliofunikwa,alipofika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwaangalia majeruhi wa ajali hiyo.

Leave A Reply