The House of Favourite Newspapers

Video: Kongamano la Familia na Nabii Bendera – Ufunuo Church

0

KANISA LA UFUNUO chini ya Mtumishi wa Mungu Askofu Paul Bendera limeandaa kongamano kubwa la Kifamilia litakalofanyika Kanisani hapa leo Jumapili ya Desemba 27, 2020.

 

Hii ni katika kufunga wiki ya familia na kufunga mwaka 2020 kwa kuikusanya familia ya Mungu pamoja, kumtukuza na kumsifu muumba wetu, huku tukipata mafundisho mahsusi kwa ajili ya familia.

 

Kwaya mbalimbali zitakuwepo ikiwa ni Pamoja na Ufunuo Gospel, waimbaji maarufu wa muziki wa injili watakuwepo.

 

Baba, Mama, dada, kaka, bibi, babu, mjomba, shangazi na wote mnakaribishwa kwenye kongamano hilo katika Kanisa la Ufunuo, (Kwa Benderea) Kimara Bonyokwa – Dar es Salaam.

 

NJOO TUJUMUIKE KUMSIFU BABA WA MBINGUNI

Leave A Reply