The House of Favourite Newspapers

Snura Akana kumwagana na Minu

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Snura’ amekanusha kuwa hajaachana na mpenzi wake Minu Calypto kama ambavyo watu wengi walikuwa wakiamini hilo.  Akizungumza na Risasi Vibes, Snura amesema kuwa anawashangaa watu kwa kujadili mapenzi ya watu ikiwa ya kwao yanawashinda.

“Eti mimi kuposti picha siku ya wapendanao nikiwa na mpenzi wangu, watu wakaanza kusema eti tumerudiana. Kwani tuliachana? Sijawahi kuachana naye, kuhusu mimi kufuta picha zake kwenye account yangu ya Instagram ni kuamua tu lakini kwa sasa penzi letu ndio kwanza limechanua,” alisema Snura.

Mwaka jana, mrembo huyo alidaiwa kuachana na mpenzi wake huyo na kufuta picha zake zote Instagram, jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa Instagram.

Leave A Reply