The House of Favourite Newspapers

Snura Ayapa Kisogo Mapenzi

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ameibuka na kusema kuwa ameamua kuyapa mapenzi kisogo kwani hayana faida kwake.

 

Akizungumza na Amani, Snura alisema baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Minu kwa sasa yupo singo na amewekeza nguvu zake zote kwenye kazi yake ya muziki zaidi.

“Kiukweli hakuna jipya kwenye mapenzi, kama watoto ninao wawili na sidhani kama kukosa mpenzi kutanifanya niwe tofauti kwa hiyo kwa sasa niko bize na kazi zangu ili niweze kuwahudumia watoto wangu pamoja na familia yangu kwa kuwa nategemewa,” alisema Snura.

Stori: Neema Adrian

Leave A Reply