The House of Favourite Newspapers

SNURA KUFUNDISHA KWAYA SHULENI

MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ameibuka na kueleza kwamba anajipanga kufundisha kwaya kwenye shule mbalimbali kwani muziki kila kukicha unazidi kuwa mgumu.

 

Snura alifikia kujipanga kufanya kazi hiyo ya kufundisha kwaya shuleni kutokana na hivi karibuni wimbo wake wa Chura kufungiwa kisa hauna maadili jambo ambalo alisema lilimchanganya kwani wao wenyewe Basata ndiyo waliomruhusu wimbo huo kupigwa kwenye vyombo vya habari baada ya kuurekebisha alipofungiwa awali mwaka 2016.

 

“Kwa sasa najifikiria kujiajiri mwenyewe zaidi na zaidi ndiyo maana najipanga niwe mwalimu wa kwaya shuleni kwa kuwa muziki wetu umekuwa mgumu sana kwa sababu mtu unafungiwa wimbo wako hata kosa halijulikani.

 

“Wakati mwingine unawapelekea kazi kabisa wanaikagua lakini wanakuja kukugeuka baadaye kama ilivyo kwangu huo Wimbo wa Chura niliubadilisha na wakaukagua na kuruhusu niite waandishi wa habari na kuwaambia mabadiliko hayo na ukaanza kupigwa kwenye vyombo vya habari lakini sasa hivi nimefungiwa tena sijui hata kosa nini,” alisema Snura.

 

Risasi Vibes

Comments are closed.