The House of Favourite Newspapers

Snura: Nitakichafua Chato Jumamosi Hii

0
Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ akikamua.

 

KIMENUKA! Mkali wa miondoko ya Mduara Bongo, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ na amefunguka kuwa,Jumamosi hii (Agosti 5) atakichafua katika uzinduzi wa hoteli ba’kubwa ya JS Motel iliopo Chato mkoani Geita.

Snura Akinukisha Dar Live, Tazama ‘Chura’ Wake Alivyosababisha Kizaazaa

Akizungumza na Showbiz Xtra, Snura alisema kuwa siku hiyo ya uzinduzi atafanya tukio ambalo si la nchi hii kutokana na alivyojiandaa pamoja na madansa wake.

“Mashabiki wote wanaifahamu shughuli yangu nikiwa katikati ya jukwaa. Tena hii imekuja mahala pake kwani nitawazindulia ngoma yangu mpya hukohuko kwenye uzinduzi wa JS Motel, asikw-ambie mtu yaani nitakin-ukisha mwanzo mwisho, kuanzia Chura, Najibadua, Shindu, Ushaharibu, Majanga na nyingine kibao.

 

Darassa akifanya yake.

 

Siku hiyo sitawaimbia tu, nitawapa staili mpya ya kucheza nyimbo hizo ikiwemo na ya sasa ya Nionee Wivu niliowashirikisha Yamoto Band,” alisema Snura ambaye atakuwa na timu yake nzima ya madensa namba moja kwa kukata ‘uno’ jijini Dar.

 

Mbali na uwepo wa Snura, siku hiyo pia mkali wa Hip Hop, Sharif Thabeet ‘Darassa’ anayebamba na Ngoma ya Hasara Roho na Muziki alisema kuwa, kwa mara nyingine anarudi Chato lakini safari hii anarudi kuonyesha burudani ya kishindo zaidi kwa kuwa itawahusisha wateja na waalikwa wote watakaofika katika uzinduzi wa JS Motel.

USIKU WA DARASSA NA ROMA, DARASSA ALIVYOISIMAMISHA DAR ES SALAAM KWA MUDA PART 02

 

“Huwa sikosei linapotokea suala la mualiko kama hili la uzinduzi. Nashukuru kuwa miongoni mwa watakaozindua JS Motel ndani ya Chato Mjini kwa mara ya kwanza na ninachoahidi kufanya makamuzi ya live jukwaani nikipiga nyimbo zangu zote ikiwemo Too Much, Sikati Tamaa, Weka Ngoma pamoja na ngoma yetu hii ya taifa ya Muziki,” alisema Darassa.

 

SHOWBIZ XTRA | AMANI

Leave A Reply