The House of Favourite Newspapers

SOKABET… Mayweather Ataingiza Mabilioni, Wewe Ingiza Mamilioni

0
Floyd Mayweather Jr.

WATU wa burudani wanamfahamu vizuri Floyd Mayweather Jr, kwani mbali na kuwa ni bondia maarufu, upande wa pili ni staa mkubwa ambaye anapenda maisha ya ‘kula bata’.

Mayweather ni mtu wa kazi kweli hasa awapo ulingoni, lakini nje ya kazi yake anapenda kuoneshea mali na fedha anazomiliki.

Mastaa wengi wa dunia katika ulimwengu wa burudani wanamtambua na wanampigia saluti katika suala hilo la kupenda maisha ya kujionesha nguvu ya fedha aliyonayo.

Sasa Jumamosi ijayo ya Agosti 26, mwaka huu. Mayweather Jr anatarajiwa kuwa ulingoni kupigana na Conor McGregor katika pambano la uzito wa Super Welterweight, ambapo mabondia wote hao wanatarajiwa kuingiza mamilioni ya dola, ambayo kwa Tanzania thamani yake ni mabilioni ya shilingi.

Wakati mabondia hao wakiingiza fedha hizo, upande wa pili wewe Mtanzania unaweza kuingiza fedha nyingi kupitia mchezo wa kubashiri matokeo katika Kampuni ya Sokabet.

Floyd Mayweather Jr na Conor McGregor.

HII IMEKAAJE?

Unachotakiwa kutambua ni kuwa siku chache zijazo Kampuni ya Sokabet inayojihusisha na kutabiri matokeo ya michezo mbalimbali inatarajiwa kuanza kazi rasmi. Pindi itakapoanza namba yako ya bahati itakuwa ni 335757 ambayo ni namba ya kampuni.

KUJIANDIKISHA NI BURE

Kujiandikisha ili uanze kubashiri mchezo wowote unaotaka ni bure kabisa.

Kwanza kabisa kitu muhimu utakachotakiwa kufanya baada ya kuanza rasmi kwa shughuli za Sokabet, utatakiwa kufungua tovuti ya ww.sokabet.co.tz kisha unabonyeza sehemu ya ‘sign up’ yaani jisajili kwa mara ya kwanza.

Hapo utajaza nafasi chache zilizo wazi, utatumiwa namba yako ya siri kwa njia ya SMS katika namba uliyojaza ambayo utaitumia kuingia ndani rasmi kuanza kubashiri.

Baada ya hapo utarejea kwenye sehemu ya kuingia ndani yaani ‘LOGIN’, utaandika namba yako ya simu na kuingiza namba ya siri uliyotumiwa kwa njia ya SMS.

Ukitaka kubashiri pambano la Mayweather Jr na McGregor, utatakiwa kuingiza fedha kwenye akaunti yako ya kubashiri ndani ya tovuti ya Sokabet.

UNAINGIZAJE SALIO

Ikiwa unatumia Vodacom, bonyeza *150*00#, chagua namba 4 (lipa kwa M-pesa), chagua namba 4 (weka namba ya kampuni), baada ya hapo ingiza namba ya kampuni ambayo ni 335757, ingiza kumbukumbu ambayo ni neno ‘Soka’.

Hapo utaingiza kiasi unachotaka, mfano Sh. 1,000 kisha malizia kwa kuweka namba yako ya siri, bonyeza namba 1 ili kukamilisha mchakato.

Ukihitaji kuingiza fedha kwa njia ya Tigopesa, bonyeza *150*01#, chagua namba 4 (lipia bili), bonyeza namba 3 (ingiza namba ya kampuni), baada ya hapo ingiza namba 335757 kisha ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuingiza (mfano Sh 1,000) kisha ingiza neno ‘Soka’, malizia na namba yako ya siri ya Tigopesa.

Utakuwa umeshajaza salio kwenye akaunti yako ya Sokabet tayari kwa ajili ya kuanza kubashiri. Ndani ya tovuti ya Sokabet utakutana na pointi (odd) 41 za kubashiri pambano hilo.

Kwa wale wanaoelewa odd 41, hizo ni kubwa kuliko maelezo, kwa ufupi, mfano ukibashiri pambano hilo moja tu, kwa kuweka shilingi 1,000 kisha ukapatia, utapata Sh. 33,800, ukiweka Sh. 5,000 unapata Sh 169,000 kwa buku tu tena hapo ni pambano moja.

Floyd Mayweather Jr.

 

SIYO NDONDI NA SOKA TU

Kampuni nyingi za michezo ya aina hiyo nchini zimeweka nguvu kwenye soka pekee, lakini Sokabet inakuja tofauti.

Kwa faida yako, baadhi ya michezo ambayo utaikuta katika tovuti ya Sokabet ni soka ambayo ni kipenzi cha wengi, American Football, baseball, kikapu, kriketi, golf, mpira wa mikono (handball), ice hockey, mbio za magari, ragbi, tenisi, volleyball na ndondi.

KUNA SH MILIONI 100 INAKUSUBIRI

Unahitaji kiwango cha shilingi 1,000 tu kupata shilingi milioni 100 kama kiwango cha juu cha kubashiri, kipengele hiki kinaitwa Sokabet Jackpot.

SH 200 INAKUJAZA MAMILIONI

Ukishaingiza fedha kwenye akaunti yako, unaweza kuanza kubashiri hata ukiwa na salio la shilingi 200 tu ambayo itakuwezesha kupata mamilioni ya fedha.

NAMBA YA BAHATI 335757

Washiriki watakuwa wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, unatakiwa kuiweka kichwani namba 335757 ambayo ni ya Sokabet, hii ndiyo itakupa neema yote ya kukufanya umiliki mamilioni ya fedha.

MAKALA: MWANDISHI WETU DAR

Leave A Reply